Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

BODI YA CHAI TANZANIA

Huduma Zetu

Majukumu ya Bodi ya Chai kama yalivyoainishwa kwenye Sheria ya Chai Nambari 3 ya mwaka 1997 kifungu kidogo cha 5 sehemu ya 3 ni kama ifuatavyo:

  1. Kuishauri Serikali juu ya sera na mikakati ya kuendeleza Tasnia ya chai nchini;
  2. Kudhibiti na kusimamia ubora wa chai na bidhaa zitokanazo na chai;
  3. Kukusanya, kuchambua na kusambaza taarifa na takwimu za chai;
  4. Kusimamia uzalishaji na uuzaji wa chai nje ya nchi;
  5. Kudhibiti usindikaji na uhifadhi wa chai pamoja na bidhaa zitokanazo na chai;
  6. Kuiwakilisha Serikali katika masuala ya kitaifa na kimataifa yanayohusu Tasnia ya Chai;
  7. Kudhibiti uingizaji wa chai nchini na uuzaji wa chai nje ya nchi;
  8. Kuhamasisha na kulinda maslahi ya wakulima ili wasipoteze haki zao kwa wanunuzi wa chai wanaoweza kujiunga kupitia vyama vya wakulima;
  9. Kudhibiti wadudu waharibifu na magonjwa katika zao la chai;
  10. Kutekeleza majukumu mengine yoyote ya kibiashara kwa idhini ya Waziri mwenye dhamana ya kilimo.