Tunachokifanya
Tunachokifanya
Majukumu ya Bodi ya Chai kama yalivyoainishwa kwenye Sheria ya Chai Nambari 3 ya mwaka 1997 kifungu kidogo cha 5 sehemu ya 3 ni kama ifuatavyo:
- Kuishauri Serikali juu ya sera na mikakati ya kuendeleza Tasnia ya chai nchini;
- Kudhibiti na kusimamia ubora wa chai na bidhaa zitokanazo na chai;
- Kukusanya, kuchambua na kusambaza taarifa na takwimu za chai;
- Kusimamia uzalishaji na uuzaji wa chai nje ya nchi;
- Kudhibiti usindikaji na uhifadhi wa chai pamoja na bidhaa zitokanazo na chai;
- Kuiwakilisha Serikali katika masuala ya kitaifa na kimataifa yanayohusu Tasnia ya Chai;
- Kudhibiti uingizaji wa chai nchini na uuzaji wa chai nje ya nchi;
- Kuhamasisha na kulinda maslahi ya wakulima ili wasipoteze haki zao kwa wanunuzi wa chai wanaoweza kujiunga kupitia vyama vya wakulima;
- Kudhibiti wadudu waharibifu na magonjwa katika zao la chai;
- Kutekeleza majukumu mengine yoyote ya kibiashara kwa idhini ya Waziri mwenye dhamana ya kilimo.