Sisi ni Kina Nani
Bodi ya Chai Tanzania (TBT) ni Taasisi ya umma iliyo chini ya Wizara ya Kilimo iliyoanzishwa kupitia Sheria ya Chai Nambari 3 ya mwaka 1997 iliyopitishwa na Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 4, 1997. TBT ilianza rasmi shughuli zake Oktoba 1, 1997.
Kufuatana na sheria hii, iliyokuwa Mamlaka ya Chai Tanzania (Tanzania Tea Aauthority - TTA) ilivunjwa na kuundwa vyombo viwili ambavyo ni Bodi ya Chai Tanzania (Tea Board of Tanzania -TBT) na Wakala wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania (Tanzania Smallholders Tea Development Agency -TSHTDA). Sambamba na uwepo wa taasisi hizi, TBT hufanya kazi kwa Karibu na Taasisi ya Utafiti wa Chai (Tea Research Institute of Tanzania-TRIT) ambayo huendeshwa kupitia ubia wa sekta binafsi na umma (PPP).