VICTORIA TEA YAFUFUA KIWANDA, WAKULIMA WA KAGERA KUUFAIKA
Bodi ya Chai Tanzania (TBT) kupitia Meneja Masoko wake, Bw. Suleiman Chillo, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa kampuni ya Victoria Tea, Dkt. Peter Mgimba, katika makao makuu ya Bodi jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yalilenga fursa za masoko zitakazonufaisha kampuni ya Victoria Tea, iliyopo mkoani Kagera ambayo awali ilijulikana kwa jina la Kagera Tea. Kiwanda hicho, ambacho kimeanza tena uzalishaji baada ya kusimama kwa muda mrefu, kimeweka mkakati wa kuzalisha chai bora na kuimarisha ushawishi wake katika masoko ya kimataifa.
Dkt. Mgimba alikumbusha kuwa mwaka 2006 kampuni hiyo iliwahi kupeleka majani ya chai nchini Japan yaliyo saidia mgonjwa wa saratani kupona.
Kurejea kwa uzalishaji wa Victoria Tea kunatarajiwa kuimarisha kipato cha wakulima wa chai wa Mkoa wa Kagera.