MAKAMU MWENYEKITI WA BODI YA CHAI AWAONGOZA WAJUMBE KUJADILI MIKAKATI YA KUINUA ZAO LA CHAI

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Chai Tanzania (TBT), Bw. Iman Kajula, ameongoza kikao cha Bodi kilichowakutanisha wajumbe wa Bodi pamoja na timu ya Menejimenti ya TBT.
Kikao hicho muhimu kimehudhuriwa na Timu ya Bodi ya Wakurugenzi Erick Jackson, Nashon Kamnyungu, Regina Kapinga, na Christon Nyagawa na timu ya Menejimenti ya TBT ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya chai Bi. Beatrice Banzi.
Wakati wa kikao hicho, Bw. Kajula amendesha majadiliano yenye lengo la kuimarisha sekta ya chai nchini, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Bodi ya Chai Tanzania katika kuinua ubora na tija ya zao hilo kimkakati.
Aidha, Bw.Imani Kajula ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo amewasisitiza wajumbe na watendaji wa Bodi kuendelea kudumisha utendaji bora, ubunifu na uwajibikaji, sambamba na kuwekeza katika mbinu bunifu zitakazoongeza thamani na ushindani wa chai ya Tanzania katika soko la ndani na nje ya nchi.