Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

BODI YA CHAI TANZANIA

Matukio mbalimbali yanayoendelea kwenye maonesho ya 12 ya Kilimo nchini Qatar ya Agritech.

Imewekwa: 12 Feb, 2025
Matukio mbalimbali yanayoendelea kwenye maonesho ya 12 ya Kilimo nchini Qatar ya Agritech.

Aidha, Bodi ya Chai imeambatana na mkurugenzi wa kampuni za Ak Confectionary za mjini Iringa ambazo zinafanya kazi ya kuchanganya na kufungasha chai (Tea Blending and Packing), ambapo amefanikiwa kufanya mazungumzo na wafanya biashara mbalimbali na kukubaliana kuhusu njia za kufanya kuileta Chai yake nchini Qatar.

Washiriki wengi wa Kongamano hilo walivutiwa na Chai yake baada ya kuonjeshwa.

Mkurugenzi wa AK Confectionery ameushukuru ubalozi wa Tanzania nchini Qatar pamoja na Bodi ya Chai kwa kushirikiana na wadau kwa kuungana nao kwenye safari za kutafuta masoko kimataifa.