Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

BODI YA CHAI TANZANIA

BODI YA CHAI YATOA MAFUNZO YA KILIMO ENDELEVU KWA WAKULIMA WA LUPEMBE.

Imewekwa: 17 Sep, 2025
BODI YA CHAI YATOA MAFUNZO YA KILIMO ENDELEVU KWA WAKULIMA WA LUPEMBE.

Bodi ya Chai Tanzania (TBT) imeendesha mafunzo ya kilimo endelevu kwa wakulima wa Lupembe ikiwa ni hatua muhimu ya kuwawezesha kupata cheti cha ithibati cha Rainforest Alliance (RA). 

Mafunzo yaliyotolewa yamejikita katika maeneo mbalimbali ikiwemo:
Utunzaji wa mazingira, Usafi wa binafsi na afya,Uhifadhi wa misitu, Haki za watoto, Kuzuia uchomaji wa misitu na mashamba, Usalama wa maji ya kunywa,Utupaji wa maji taka,pamoja na kanuni nyingine za kilimo endelevu.

Jumla ya wakulima 2,755 kutoka vijiji mbalimbali wanashiriki, wakiwemo: Igombola (330), Ihang’ana (64) Isoliwaya (398),Kanikelele (761) Kitole (177),Lupembe (225) Lialalo (98), Matebwe (94) Nyave (68),Ukalawa (317)

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Bi. Mwalilei Mdoe, Afisa Kilimo Mwandamizi kutoka Bodi ya Chai, kwa kushirikiana na maafisa wa NOSC akiwemo Ivan Massawe, Imanuel Kingiliilwe na Mapenzi Shagama.