TBT yakutana na viongozi wa ushirika

Bodi ya Chai Tanzania(TBT) imekutana na Viongozi wa Vyama vya Ushirika katika Sekta ya Chai ili kusikiliza maoni yao yanayolenga kuboresha utendaji kazi baada ya kuunganishwa kwa Wakala wa Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania(Tishtida) na TBT.
Katika kikao hicho kilichofanyikia katika Makao Makuu ya TBT, Dar es Salaam na kuongozwa na Kaimu Mkurungenzi wa TBT, Bi. Beatrice Banzi viongozi hao wameunga mkono hoja ya muungano huo.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Kaimu Mkurugenzi wa TBT Beatrice Banzi amewataka viongozi hao kutambua nia ya dhati ya serikali ya kuziunganisha Taasisi hizo ni kuimarisha ufanisi zaidi katika sekta ya chai.
Amesema, baada ya kuunganishwa Tishtida itakuwa ni idara katika TBT huku pia ikianzishwa kampuni tanzu itakayokuwa ikifanya kazi kibiashara.
Amesema,"Nawapongeza kwa kuja kushiriki katika kutoa maoni yenu juu ya kuunganishwa huku, na niwahakikishie kuwa chini ya kuunganishwa huku hakuna kitakachoharibika isipokuwa ufanisi utazidi kuimarika zaidi na sekta itazidi kukua"
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Wakulima wadogo wa Chai, Sakari cha mkoani Tanga, Felix Chole jambo muhimu na pia sheria katika chai zibadilishwe kuendana na wakati ili kuihudumia sekta hiyo.
Pia ametaka maboresho yanayofanyika kumnufaisha mkulima mdogo wa chai hapa nchini.