Tanzania na Japan kushirikiana kuendeleza sekta ya chai

Wataalamu wa sekta ya chai kutoka nchini Japan wamewasili hapa nchini kwa ziara ya siku saba ambapo wakiwa nchini wanatarajiwa kutembelea mikoa ya Iringa na Njombe kutembeela wadau wa chai wakiwemo wakulima wa zao hilo.
Wajapan hao wanawakilisha kampuni kubwa kutoka Japan ambazo ni Kawasaki Kiko ikiongozwa na Bw. Hirofumi Suganuma na kampuni nyingine ni Nasa Corporation.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBT. Bi, Beatrice Banzi amesema kuwa ugeni wa wataalamu hao ni matokeo chanya ya harakati za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dk Samia Suluhu Hassan zinazolenga kuboresha sekta mbalimbali za kimkakati hapa nchini.
Anasema wataalamu hao wamewasili kufuatilia sekta ya chai kwa lengo la kuanza uwekezaji ambao amesema kuwa utakuwa na manufaa makubwa kwa wakulima wa chai hapa nchini.