CHAI YA TANZANIA YAWAVUTIA WENGI KWENYE MAONESHO YA UTALII NCHINI JAPAN
CHAI YA TANZANIA YAWAVUTIA WENGI KWENYE MAONESHO YA UTALII NCHINI JAPAN
Imewekwa: 29 Sep, 2025
Picha ikionesha Ubalozi wa Tanzania nchini Japan ulivyoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Utalii yaliyofanyika nchini humo kuanzia tarehe 25 hadi leo, 28 Septemba 2025.
Katika maonesho hayo, Ubalozi wa Tanzania umeonesha vivutio vya kipekee vya utalii vinavyopatikana nchini Tanzania, huku banda la hilo likipambwa na uonjaji wa chai ya Tanzania. Hatua hiyo iliwavutia wageni wengi waliotembelea maonesho hayo na kuwapa fursa ya kufahamu ubora na ladha ya kipekee ya chai ya Tanzania.