Balozi wa Urusi nchini ateta na Kaimu Mkurugenzi wa TTB

Balozi wa Shirikisho la Urusi Mheshimiwa Andrey Avetsyan atembelea Bodi ya chai Tanzania na Kupokelewa na Kaimu Mkurugezi wa Bodi ya Chai Bi. Beatrice Banzi, Kwa lengo la kuangalia fursa za uwekezaji zilizopo kwenye mnyororo wa thamani wa zao la chai.
Mkurugezi Mkuu Bi Beatrice alielezea kuwa fursa zilizoko kwenye zao la chai ni uwekezaji katika 1. Viwanda vya kuchakata chai, viwanda vya kuchanganya na kufungasha chai, 2. Uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza vifungashio vya chai na 3. Kuwekeza kwenye teknolojia za kukuza uzalishaji wa chai
Sambamba na hayo Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya chai Alisema Bodi ipo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa chai Nchini.
Aidha Mheshimiwa Balozi alivutiwa kwa maelezo ya kina kutoka Bodi ya chai na kusema kuwa Urusi imekuwa ikishirikiana na Tanzania tangu enzi za uhuru katika nyanja mbalimbali lakini sasa urusi itaendelea kukuza diplomasia ya kiuchumi kati ya Nchi ya Tanzania na Urusi kupitia uwekezaji katika zao la chai nchini.
Ujio wa Balozi huyo ni matokeo ya jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya Kilimo chini ya waziri Hussein Bashe ikiwa na lengo la kuongeza thamani ya zao la chai ndani na nje ya nchi