Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

BODI YA CHAI TANZANIA

Kampuni kubwa za Chai kutoka Japan, ziitwazo ITO EN Ltd na Nasa Corporation zimeshawasili Tanzania

Imewekwa: 27 Mar, 2025
Kampuni kubwa za Chai kutoka Japan, ziitwazo ITO EN Ltd na Nasa Corporation zimeshawasili Tanzania

Wakurugenzi wa Kampuni kubwa mbili za chai kutokea nchini Japan, ITO EN Ltd na Nasa Corporation wametembelea kampuni ya Udzungwa Bottlers Limited ambayo inazalisha chupa na kuuza maji aina ya Udzungwa.

Lengo ni kutembelea kampuni hiyo na kuangalia maeneo ya ushirikiano ya kibiashara ambapo, bidhaa za chai ya kijani ya ITO EN mara nyingi huwekwa kwenye chupa za plastiki ambazo kiwanda cha Udzungwa pia kinaweza kuzalisha chupa hizo. Hatua hii itasaidia kampuni ya ITO EN kuwekeza Tanzania lakini pia kugusa na kunufaisha wazawa wa Tanzania wanaofanya biashara katika mnyororo wa thamani wa zao la chai kwenye chupa za plastiki.

Sambamba na hayo baada ya kuzunguka kiwanda kidogo cha Udzungwa Bottlers Limited kilichopo mikocheni eneo la viwanda Dar es salaam, wawekezaji hao waliridhika na maelezo waliopatiwa na kuahidi kuendeleza mazungumzo kwa njia ya barua pepe kwa ajili ya kuanzisha rasmi mashirikiano ya kibiashara.

Aidha Mkurugenzi wa kampuni ya Udzungwa Bottlers Limited Bw. Anthony ameishukuru Bodi ya Chai chini ya Kaimu Mkurungenzi wake Bi. Beatrice Banzi kwa kuwa kifua mbele katika kusaidia kuleta wawekezaji kwenye sekta ya Chai ya Tanzania ambapo itagusa pia uwekezaji na upatikanaji wa ajira kwa Watanzania.