Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

BODI YA CHAI TANZANIA

Wataalamu wa chai wa Japan wakutana na Naibu Katibu Mkuu Kilimo

Imewekwa: 14 Dec, 2024
Wataalamu wa chai wa Japan wakutana na Naibu Katibu Mkuu Kilimo

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao. Dk, Hussein Mohamed Omar amewataka wawekezaji kuzidi kujitokeza kuwekeza kwenye sekta ya chai ili kuiwezesha sekta hiyo kuzidi kuchangia pato la taifa.

Dk. Mohamed amesema hayo wakati alipokutana na timu ya wataaamu kutoka kampuni za Kawasaki Kiko na Nasa Corporation zote za nchini Japan.

Dk. Omar amesema iwapo wawekezaji wakijitokeza kwa wingi zaidi kuwekeza kwenye mnyororo mzima wa chai hususan katika kufungua viwanda vya uchakataji na ufungashaji wakulima wengi wa chai watanufaika.

Anasema,"sekta ya chai ina fursa lukuki na zote hizi zinaweza kuiinua sekta hii, hivyo ni imani ya wizara kuwa kampuni zenu hizi za Japan kwa kuwa ni za uchakataji na ufungaji hakika na zikinunua moja kwa moja chai za wakulima ni hakika wakulima watakuwa na soko la uhakika na wigo mpana zaidi wa kuuza chai zao." 

Ujumbe huo wa wataalamu watano kutoka kampuni hizo za Japan unaongozwa na Bw. Hirofumi Suganuma, Mkurugenzi wa Miradi ya Maendeleo, Kampuni ya Kawasaki Kiko ya Japan.