Dk Omar awasihi wafanyakazi wa TBT kuendelea kupiga kazi
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula, Dk.Hussein Mohamed amekutana na Wafanyakazi wa bodi ya Chai Tanzania(TBT) na kuwasisitizia kuendelea kufanya kazi kwa bidii.
Katika kikao hicho kilichofanyika katika Makao Makuu ya TBT na kuhudhuriwa na Wafanyakazi akiwemo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wake, Bi.Beatrice Banzi, Dk. Omar amewataka wafanyakazi hao kuhakikisha kuwa ufanyaji kazi kwa bidding na ubunifu utawezesha ufanisi zaidi katika kusimamia zao la chai.
Dk.Omar pia ameitaka Bodi ya Chai kuhakikisha kuwa uzalishaji wa chai unaongezeka maradufu hapa nchini ili kuiwezesha sekta hiyo kuendelea kuchangia kikamilifu kwenye pato la taifa.
Katika kuhakikisha adhma hiyo ya sekta ya chai kuchangia pato la taifa, Dk Omar ameitaka TBT kufanikisha kilimo cha umwagiliaji katika zao la chai hatua itakayoongeza ukuaji wa zao hilo.
"Nawasihi kuhakikisha kuwa mnasimamia kwa ufanisi zao hili ili kuhakikisha wakulima wanalima na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa chai hapa nchini, lakini pia bodi mnatakiwa kuendelea kusaka masoko ya ndani na nje ya nchi." amesema Dk.Omar.
Naye Bi. Beatrice amemhakikishia Dk.Omar kuwa bodi hiyo na Wafanyakazi wake wa ujumla wamejipanga kutekeleza kikamilifu maagizo yaliyotolewa.
#chaiyetufahariyetu