Naibu Katibu Mkuu- Kilimo, Dk. Omar akutana na wawakilishi wa wawekezaji kutoka China
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dk. Hussein Omar Mohamed amekutana na wawakilishi wa kampuni ya kichina inayojihusisha na kilimo kujadiliana mwendelezo wa jitihada zao za kusaka maeneo ya uwekezaji katika sekta ya chai hapa nchini.
Kampuni hiyo ya Hong Ding Xin imejikita katika Mkoa wa Iringa Wilaya ya Kilolo pamoja na Mbeya ikisaka maeneo ya kuwekeza katika sekta ya Chai.
Kikao na Wachina hao pia kimehudhuriwa na Kaimu Mkurungenzi wa Bodi ya Chai Tanzania(TBT), Bi. Beatrice Banzi, Mratibu wa Mradi wa Bulding A Better Tomorrow(BBT), Vumilia Zekankuba na Mkurugenzi wa Idara ya Matumizi Bora ya Ardhi, Injinia. Juma Mdeke na Injia Makori.
Katika kikao hicho Dk Omar alipata wasaha wa kusikiliza taarifa ya TBT kuhusiana na uwekezaji wa wachina hao pamoja na namna ambavyo wizara imejipanga kufanikisha uwekezaji wao.
Pia alisikiliza namna ambavyo wachina hao wameshatembelea na kutambua maeneo ya uwekezaji wao wanaotaka kuwekeza katika sekta ya chai.