Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

BODI YA CHAI TANZANIA

"Leteni chai mnadani ndo mpate Vibali" Mkurugenzi Mkuu TBT

Imewekwa: 06 Jun, 2025
"Leteni chai mnadani ndo mpate Vibali" Mkurugenzi Mkuu TBT

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania(TBT), Beatrice Banzi amesema kuwa Ofisi yake haitotoa kibali cha kusafirisha majani ya chai nje ya nchi kwa kampuni yoyote ambayo haitowasilisha asilimia 15 ya majani yake kwenye mnada wa chai wa hapa nchini.

"Najua mnafahamu kuwa chai ya Tanzania ni bora tena sana na ninashangaa kusikia kuwa wapo ambao wanaibeza na wengine ni kampuni za hapahapa nchini ambazo zinapeleka chai katika mnada wa Mombasa lakini kwa huu wa hapa nchini zinaleta chai zisizo na ubora sasa mimi sitakuwa na mzaha na watu kama hawa." amesema Mkurugenzi Beatrice.