Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

BODI YA CHAI TANZANIA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBT akutana na wadau wa chai kutoka Misri

Imewekwa: 29 Nov, 2024
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBT akutana na wadau wa chai kutoka Misri

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania (TBT), Beatrice Banzi amekutana na Wadau wa Sekta ya Chai kutoka nchini, Misri ambapo kwa pamoja wamejadiliana masuala mbalimbali kuhusiana na sekta ya chai ikiwa ni pamoja na kushiriki kwenye maonesho ya chai yatakayofanyika nchini humo mapema mwakani.