Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

BODI YA CHAI TANZANIA

Mtaalamu wa Chai kutoka Bodi atembelea shamba la chai

Imewekwa: 19 Jan, 2025
Mtaalamu wa Chai kutoka Bodi atembelea shamba la chai

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Machare Estate, Madam Bente ( katikati) akiwa na Meneja wake(kushoto) pamoja na Mtaalamu kutoka Bodi ya Chai Tanzania (TBT) wakati Mtaalamu huyo alipotembelea shamba la Machare.

 

Kampuni hiyo ya Machare Estate inamiliki kiwanda cha kuchakata majani mabichi ya chai kwa ajili ya  kupata chai kavu maalumu yaani orthodox tea.

 

Akiwa katika kiwanda hicho alipata wasaha wa kutembelea Maabara ya Chai iambapo ndani yake ndipo chai inaandaliwa kwa ajili ya uonjaji baada ya kutengenezwa.

 

Pia alipata wasaha wa kuona chai mbalimbali zikiwemo ambazo hazijafanyiwa uchachuaji yaani "unfermented tea" pamoja na zile ambazo zimefanyiwa uchachuaji " fermented teas'".