Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

BODI YA CHAI TANZANIA

Tanzania na Sudan kufufua ushirikiano wa kibiashara katika sekta ya chai

12 Jun, 2024 - 12 Jun, 2025
15:21:00 - 15:24:00
Masaki
evancengingo@gmail.com +255714436594

Historia kubwa na ya muda mrefu ya ushirikiano wa kibiashara kwenye sekta ya chai kati ya Tanzania na Sudan inaenda kuandikwa upya, kutokana na harakati zinazofanywa na Bodi ya Chai Tanzania( TBT) chini ya uongozi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Bi. Beatrice Banzi.

Sudan imekuwa mnunuzi mkubwa wa chai ya Tanzania tangu miaka ya 70, kabla ya kuacha kununua chai hiyo ambapo kwa sasa kupitia mazungumzo na TBT, Balozi wa Sudan hapa nchini, Mohamed Abdalla Abdulhamid nchi hizi mbili zinaenda kufungua tena ushirikiano huo.

Nchi ya Sudan ambayo kati ya tamaduni zake ni pamoja na unywaji wa chai,    ambapo kwa mujibu wa balozi huyo mwananchi wa Sudan hunywa vikombe vinne hadi vitano vya chai kwa siku na hivyo kuwa ni kati ya soko lenye uhitaji mkubwa zaidi wa bidhaa hiyo.

Katika mazungumzo kati ya balozi huyo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBT, Bi.Beatrice Banzi yaliyofanyika katika Ofisi za Ubalozi huo, Dar es Salaam, Mh. Balozi Abdulhamid amebainisha kuwa kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1970 mwanzoni wa miaka ya 90 Sudani ilikua ikinunua kwa wingi chai ya Tanzania na asilimia 90  ya chai iliyokuwa ikitumiwa na  wananchi wa Sudan ilikuwa ikitoka Tanzania.

"Nikiwa kijana mdogo nilikuwa nakunywa sana chai kutoka Tanzania na ndiyo ilikuwa chai inayopendwa Sudan, nakumbuka kulikuwa na maboksi makubwa ya chai hiyo ila kwa baadae ikapotea na ninafurahi kwa uamuzi wa bodi yenu kuja ili tufufue biashara hii" amesema, Mh.Balozi Abdulhamid

Katika kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na Meneja Masoko ya Ndani na Nje ya Nchi wa TBT, Bw.Selemani Chillo kimelenga kufungua njia mpya ya biashara ya Chai kati ya Tanzania na Sudan ikiwa ni pamoja na kurudisha mahusiano ya kibiashara kwenye Chai kati ya nchi hizo.

Mh. Balozi ameahidi kushirikiana na Bodi ya Chai katika kuunganisha wanunuzi na wawekezaji wakubwa watakaofanya biashara na kuwekeza kwenye Sekta ya Chai hapa nchini.

Kaimu Mkurugenzi wa TBT, Bi. Beatrice amemhakikishia ushirikiano mkubwa balozi huyo huku akibainisha kuwa Tanzania inazo fursa nyingi za Uwezekaji katika tasnia ya chai.

Amezitaja fursa hizo kuwa ni pamoja ufungashaji, uchakataji na uzalishaji wa chai huku akibainisha kuwa wawekezaji kutoka Sudan wanaweza kuchakata chai ya Tanzania na kuuza kokote duniani kwa kuwa soko ni zur

Tanzania na Sudan kufufua ushirikiano wa kibiashara katika sekta ya chai