Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

BODI YA CHAI TANZANIA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBT akutana na wadau wa chai kutoka Misri

Katika harakati zake za kuliendeleza zao la chai hapa nchini hasa kwa kufungua mipaka zaidi ya kibiashara leo Novemba Mosi, Bodi ya Chai Tanzania (TBT) imekutana na uongozi wa Kampuni ya National Training Academy ya nchini Misri. Kampuni hiyo inaandaa Tamasha la Africa la Chai na Kahawa litakalofanyika February mwakani nchini Misri likiwa na lengo la kukutanisha wadau mbalimbali mazao hayo kutoka nchi za Afrika. Ujio wa watendaji kutoka kampuni hiyo umelenga kuikaribisha TBT kushiriki katika Kongamano hilo pamoja na kuyafungua masoko ya chai katika nchi za ukanda wa Afrika ya Kati na nchi za karibu za ukanda wa waarabu. Ugeni huo uliopokelewa na Kaimu Mkurungenzi wa TBT, ulipata wasaha wa kuonja Chai Maalum (Orthodox Tea) ambayo ni kati za chai zinazozalishwa hapa nchini na na waliifurahia chai hiyo. Kutokana na kuvutiwa na uandaaji wa chai hiyo, wameamua kuwatembelea wazalishaji wake kwa lengo la kubainisha namna ya uandaaji wake na kujadiliana nao njia bora ya kuifikisha chai hiyo katika nchi za Ukanda tajwa Akizungumzia ugeni huo, Kaimu Mkurugenzi wa TBT, Bi. Beatrice ya Chai anasema," leo tumepokea ugeni huu wa wadau muhimu wa chai na tumezungumza juu ya ushirikiano wetu katika kuiendeleza sekta ya chai kwa kupata Wawekezaji na Masoko ya chai katika Ukanda wa Afrika ya Kati na Nchi jirani za ukanda wa Uarabuni."